Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (a.s) - ABNA - Kufuatia mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni, Baraza la Uratibu wa Tabligh za Kiislamu limetoa taarifa likiwaalika Wananchi watukufu wa Tehran kushiriki maandamano hayo yatakayofanyika kesho katika Medani ya Palestina.
Nakala ya tangazo hilo ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Katika siku za giza ambapo wananchi madhlumu wa Ghaza wanapigana bila kuchoka vita visivyokuwa vya usawa na utawala wa Kizayuni, jambo ambalo limesababisha kuuawa Shahidi idadi kubwa ya watu wasio na ulinzi na waandishi wa habari waliopo Palestina na maiti zao zikiruka angani, huku kwa upande mwingine, mzingiro, njaa na kulengwa / kushambuliwa kwa magari ya wagonjwa na wafanyakazi wa afya, uga huo umefifia kwa Wananchi wa Palestina wanaodhulumiwa na wenye kufanya Muqawamah / mapambano ya upinzani.Wananchi hawa wanaodhulumiwa na kukandamizwa wa Ghaza wanashuhudia mashambulizi ya mabomu, mauaji ya halaiki na kuuawa Shahidi wapendwa wao kila wakati.
Katika mazingira haya, kukaa kimya na kuridhika ni usaliti wa historia ya Mwanadamu. Kwa vile sasa macho ya walimwengu, mashirika ya kimataifa na Baraza la Usalama yamefumbia macho jinai za utawala wa Kizayuni na Waziri Mkuu wake mbwa mwitu na mtenda jinai katika mauaji ya umwagaji damu ya watu wa Ghaza, Utawala ulioshindwa na uliokata tamaa (wa kizayuni) unaendelea na vitendo vyake vya kutisha na vya kikatili kwa nguvu zaidi. Ni wajibu wa kila Mwislamu na kila mtu anayehusika kufanya kila awezalo ili kukomesha mauaji haya, na jumuiya ya kimataifa izinduke kwa umoja dhidi ya dhulma, ukandamizaji na ukatili huu wote.
Kwa mantiki hiyo, Baraza la Uratibu wa Tabligh za Kiislamu linawaalika umma mtukufu wa Tehran kushiriki katika maandamano yatakayofanyika Jumatano, Aprili 10, saa 10 alfajiri katika Medani ya Palestina, ili kueleza masikitiko yao (na mshikamano wao) kwa Wananchi wa Palestina na kuonyesha hasira zao na kuchukizwa kwao na jinai za kinyama za utawala huo wa kizayuni wenye kiini kichafu na wakala wa Amerika katika eneo la Kikanda (Mashariki ya Kati).
Amani iwe juu yenu, na Rehema za Mwenyezi Mungu na Baraka Zake.
Your Comment